Na Balozi wa Urusi nchini Tanzania Mh Balozi YURI POPOV

Katika kuendeleza Adhma ya Serikali ya awamu ya Nane ya Sera ya UCHUMI WA BLUE nimekutana na Balozi wa Urusi nchini Tanzania Mh Balozi YURI POPOV ambae pamoja na mambo mengine tumeongea jinsi ya kuisadia Mkoa wa Kaskazini katika suala zima la utalii na pia kusaidia Maendeleo ya Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini kupitia uchumi wa Bahari,Nilimuhakikishia Mh Balozi kua Mkoa wa Kaskazini na Zanzibar kwa ujumla ni sehemu Salama kwa Watalii wanaotoka Urusi na Maeneo mengine dunia na kua Serikali ya Mkoa itahakikisha inaweka mazingira Salama ya Uwekezaji kwa wale watakaopenda kuja kuwekeza katika Mkoa huu.Katika hatua nyingine Balozi Yuri amesema kua,ameridhisha na hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya nane katika kukuza na kusimamia yema Sekta ya utalii na kua Tayari amewasiliana na viongozi kadhaa wa Urusi na kuwahakiishia kua Zanzibar ni sehemu salama kwa Watalii kutoka Urusi na kuahidi kua nchi yake itashrikiana na Serikali ya Mapinduzi katika kukuza utalii ili kuinua hali za wananchi waishio katika maeneo yanayofanya biashara ya Utaliii hususan Mkoa wa Kaskazini.

One thought on “Na Balozi wa Urusi nchini Tanzania Mh Balozi YURI POPOV

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X