Mkoa wa Unguja Kaskazini ni mmojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye Postikodi namba 73000[1]. Uko kisiwani Unguja ambayo ni kisiwa kikubwa cha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Makao makuu ya mkoa yako Mkokotoni. Kuna wilaya mbili ambazo ni Kaskazini Unguja 'A' na Kaskazini Unguja 'B'. Eneo la mkoa ni km² 470 ambako kuna jumla ya wakazi 187,455 wakiwemo 105,780 wa Kaskazini 'A' na 81,675 wa Kaskazini 'B' kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012[2]. Wengi wanajishughulisha na uvuvi na kilimo. Sehemu ya mashariki ya mkoa kuna kilimo cha karafuu. Upande wa magharibi utalii umeanza kuwa muhimu. Eneo la Ras Nungwi ni sehemu moja yenye mahoteli ya watalii wa nje.

Kisiwa cha Tumbatu ni sehemu ya mkoa huu. Miji ya mkoa ndiyo Mkokotoni, Mahonda na Gamba.

X